Luke 18:35-43

Yesu Amponya Kipofu Karibu Na Yeriko

(Mathayo 20:29-34; Marko 10:46-52)

35 a bYesu alipokuwa anakaribia Yeriko, kipofu mmoja alikuwa ameketi kando ya njia akiomba msaada. 36Kipofu huyo aliposikia umati wa watu ukipita, akauliza, “Kuna nini?” 37 cWakamwambia, “Yesu wa Nazareti anapita.”

38 dAkapaza sauti, akasema, “Yesu, Mwana wa Daudi, nihurumie!”

39 eWale waliokuwa wametangulia mbele wakamkemea, wakamwambia akae kimya. Lakini yeye akapaza sauti zaidi, “Mwana wa Daudi, nihurumie!”

40Yesu akasimama, akawaamuru wamlete huyo mtu kwake. Alipokaribia, Yesu akamuuliza, 41“Unataka nikufanyie nini?”

Akajibu, “Bwana, nataka kuona.”

42 fYesu akamwambia, “Basi upate kuona. Imani yako imekuponya.” 43 gAkapata kuona saa ile ile, akamfuata Yesu, huku akimsifu Mungu. Watu wote walipoona mambo hayo, nao wakamsifu Mungu.

Copyright information for SwhNEN